Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la China atoa wito wa uhusiano wa karibu zaidi kati ya China na Uganda
2021-10-22 08:57:54| CRI

Mwenyeiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China Li Zhanshu amefanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Uganda Jacob Oulanyah kwa njia ya video, na kutoa wito wa kuwa na uhusiano wa karibu kati ya nchi hizo mbili.

Bw. Li amesema, China iko tayari kufanya kazi na Uganda katika kutelekeza makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa nchi hizo mbili, kutumia fursa ya mkutano ujao wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika kuimarisha umoja na uratibu, na kwa pamoja kukabiliana na changamoto mbalimbali ili kuwanufaisha zaidi watu wa nchi hizo mbili.

Kwa upande wake, Oulanyah ameishukuru China kwa misaada yake na uungaji mkono, na kusema bunge la Uganda liko tayari kuimarisha mawasiliano na Bunge la Umma la China ili kuboresha mawasiliano ya pande mbili na kuimarisha ushirikiano katika nyanja mbalimbali.