Msomi wa Afrika Kusini: FOCAC inaboresha hali ya kuaminiana na uhusiano kati ya watu wa Afrika na China
2021-10-22 11:38:25| CRI

Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Afrika na China katika Chuo Kikuu cha Johannesburg David Monyae amesema, Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC limehimiza biashara na uwekezaji, na kuboresha hali ya kuaminiana na uhusiano kati ya watu wa pande hizo mbili.

Bw. Monyae ametoa kauli hiyo kwenye Kongamano la Mtandaoni (Kongandao) kuhusu FOCAC lililofanyika jana Alhamisi.

Msomi huyo amesema    FOCAC imekuwa utaratibu muhimu kwenye jukwaa la kimataifa, ambao umeboresha kidhahiri uhusiano wa kiuchumi na kati ya watu wa China na Afrika.