Uwekezaji wa China katika nchi za “Ukanda Mmoja, Njia Moja” waongezeka katika robo tatu zilizopita za mwaka huu
2021-10-22 08:45:31| CRI

Msemaji wa Wizara ya Biashara ya China Bibi Shu Jueting jana amesema, katika robo tatu ya kwanza ya mwaka huu, uwekezaji wa moja kwa moja wa China usio wa kifedha katika nchi za nje umeendelea kwa utulivu, na ushirikiano wa uwekekaji na nchi za “Ukanda Mmoja, Njia Moja” umeongezeka.

Bibi Shu amesema kati ya mwezi Januari hadi Septemba, uwekezaji wa moja kwa moja usio wa kifedha kwa nchi hizo umefikia dola za kimarekani bilioni 14.87, ambayo ni ongezeko la asilimia 14.2 kuliko mwaka jana wakati kama huo, na thamani ya miradi ya kandarasi katika nchi hizo imefikia dola za kimarekani bilioni 61.8, ikiongezeka kwa asilimia 16.3.