Raia milioni 25 wa Kenya wahitaji matibabu ya magonjwa ya kitropiki yanayopuuzwa
2021-10-22 11:38:51| CRI

Wizara ya Afya ya Kenya imesema raia wapatao milioni 25 wanahitaji matibabu ya magonjwa ya kitropiki yanayopuuzwa.

Akiongea kwenye mkutano wa Shirikisho la Huduma za Afya la Kenya (KHF) uliofanyika Nairobi, katibu mkuu mtendaji wa Wizara ya Afya ya Kenya Rashid Aman amesema magonjwa hayo yanaenea nchini kote, haswa kwenye maeneo maskini ya vijijini, ambako ni vigumu kupata maji safi na huduma za usafi.

Ofisa huyo amesema, inawezekana kwa Kenya kutimiza lengo la kutokomeza magonjwa ya kitropiki yanayopuuzwa katika miaka kumi ijayo na kuwawezesha mamilioni ya wakenya kuishi maisha mazuri bila kusumbuliwa na magonjwa hayo yanayoweza kusababisha ulemavu.