Kiwanda haramu cha kusafisha mafuta chalipuka kusini mwa Nigeria na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 25
2021-10-25 09:25:33| cri

Kiwanda haramu cha kusafisha mafuta kilichoko kusini mwa Nigeria kililipuka jana, na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 25, wakiwemo watoto.

Kwa mujibu wa ofisa wa huko, makumi ya nyumba zilizoko karibu na kiwanda hicho pia zimeharibiwa, na watu wengi wamejeruhiwa na kupelekwa hospitali. Habari zimesema viwanda vingine haramu kadhaa pia viko kwenye eneo hilo, na vinatishia usalama.