Polisi nchini Uganda yaelezea mlipuko wa bomu mjini Kampala ni kitendo cha ugaidi wa ndani
2021-10-25 09:46:07| cri

Polisi nchini Uganda yaelezea mlipuko wa bomu mjini Kampala ni kitendo cha ugaidi wa ndani_fororder_乌干达

Polisi nchini Uganda jana ilielezea mlipuko wa bomu uliotokea Jumamosi usiku katika mji mkuu wa Kampala kuwa ni kitendo cha ugaidi wa ndani.

Kwenye taarifa yake msemaji wa polisi Fred Enanga, amesema watu watatu walijifanya kama wateja kwenye sehemu ya kula huko Komamboga kiunga cha Kampala, na kulipua bomu baada ya kuondoka kwenye eneo la tukio. Bw. Enanga amefafanua kuwa mmoja wao alikuwa amechukua mfuko wa plastiki uliokuwa na vifaa visivyojulikana ambapo aliuweka chini ya meza. Watuhumiwa hao walikuwa karibu na wateja wengine na kuwanunulia vinywaji na vitafunio na baadaye kutoweka na kuuacha mfuko kwenye eneo la tukio.

Kwa mujibu wa wataalamu wa polisi bomu hilo lilitengezwa kwa vifaa vya kienyeji vikiwemo misumari na vingine vya chuma. Amebainisha kuwa wachunguzi wameshapata fununu ya kuweza kuwatambua wahusika hao watatu na sababu ya kufanya ugaidi bado haijajulikana.