Huduma za madeni ya nje za Kenya zapungua kutokana na Mpango wa wa nchi za G20
2021-10-26 09:10:46| cri

Huduma za madeni ya nje za Kenya zapungua kutokana na Mpango wa wa nchi za G20_fororder_VCG41N824337452

Ulipaji wa madeni ya nje wa Kenya kwa asilimia, kwenye huduma ya jumla ya madeni umepungua katika mwaka wa fedha wa 2020/2021 ikilinganishwa na mwaka wa nyuma yake wakati nchi hiyo ikinufaika na Mpango wa Kusitisha Huduma za Madeni wa nchi za Kundi 20 (G20).

Kwenye ripoti yake ya mwaka ya madeni iliyotolewa jana Jumatatu, Hazina ya Taifa imesema huduma ya madeni ya shilingi trilioni 7.8 za Kenya (sawa na dola za kimarekani bilioni 70) iliongezeka kutoka dola bilioni 5.9 za Kimarekani kwenye mwaka wa fedha 2019/2020 hadi dola bilioni 7 za mwaka wa fedha wa 2020/21. Hata hivyo hazina imesema katika kipindi hicho, huduma za madeni ya nje kwa asilimia ya jumla ya huduma ya madeni ilipungua kutoka asilimia 34.3 hadi asilimia 30.1, huku huduma za madeni ya ndani zikipanda kutoka asilimia 65.7 hadi 69.9.

Kupungua kwa huduma ya madeni ya nje kulichangiwa na kusitishwa kwa huduma ya madeni chini ya Mpango wa Kusitisha Huduma za Madeni wa nchi za Kundi 20.