Watu zaidi ya 17 wauawa kwenye mashambulizi vijijini nchini Nigeria
2021-10-26 09:12:01| cri

Watu zaidi ya 17 waliuawa jana Jumatatu kwenye mashambulizi katika vijiji viwili vilivyopo eneo la Mashengu, jimboni Niger, kaskazini ya kati mwa Nigeria.

Mkuu wa polisi wa jimbo hilo Monday Kuryas ameviambia vyombo vya habari kuwa genge la watu wenye silaha jana alfajiri waliingia kwenye msikiti wa kijiji kimoja, kilichopo eneo la Mashengu, wakiwapiga risasi wanavijiji waliomo ndani na kusababisha vifo vya watu, na pia kulikuwa na watu saba waliotekwa nyara. Kwa mujibu wa uchunguzi wa awali, hili lilikuwa ni tukio la kulipiza kisasi, na polisi wamewekwa kulinda kijiji hicho. Lakini Kuryas hakueleza kuhusu shambulizi lililotokea katika kijiji kingine.

Katika miezi kadhaa iliyopita, mashambulizi ya kutumia silaha yametokea mfululizo nchini Nigeria na kusababisha watu wengi kuuawa na kutekwa nyara. Tarehe 20, mwezi huu, watu 14 walitekwa nyara baada ya watu wenye silaha kushambulia basi moja.