Katibu mkuu wa UM alaani mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea nchini Sudan
2021-10-26 09:11:36| cri

Katibu mkuu wa UM alaani mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea nchini Sudan_fororder_VCG111354689678

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani mapinduzi ya kijeshi yanayoendelea nchini Sudan.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Guterres amesema waziri mkuu wa serikali ya mpito ya Sudan Abdallah Hamdok na maofisa wengine wote wa serikali walioshikiliwa ni lazima waachiliwe huru mara moja, ili kuheshimu mpango wa kipindi cha mpito uliofikiwa kwa juhudi kubwa.

Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat ametoa wito wa kurejesha mara moja mazungumzo kati ya raia na makundi ya kijeshi nchini Sudan chini ya Azimio la Kisiasa na Amri ya Kikatiba.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin amesema China inafuatilia hali mpya ya Sudan, akizitaka pande zote zinazohusika za Sudan kuondoa tofauti zao kupitia mazungumzo, na kulinda amani na utulivu wa nchi. Pia ameeleza kuwa hivi sasa ubalozi wa China nchini Sudan unafanya kazi kama kawaida, na kwamba China itachukua hatua zinazohitajika kulinda usalama wa mashirika na raia wa China nchini humo.

Marekani imesitisha msaada wa fedha wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 700 kwa Sudan baada ya jeshi la nchi hiyo kuwashikilia maofisa wa serikali ya kiraia na viongozi wengine wa kisiasa akiwemo waziri mkuu Abdallah Hamdok.