UM wasema ufikaji wa msaada wa kibinadamu katika maeneo ya kaskazini mwa Ethiopia bado una changamoto
2021-10-27 09:14:52| cri

Ofisi ya Uratibu wa Mambo ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) jana ilisema ufikaji wa msaada wa kibinadamu katika maeneo ya kaskazini mwa Ethiopia bado una changamoto.

Ofisi hiyo imesema hali ya kibinadamu katika eneo la Tigray imekuwa mbaya zaidi kutokana na vizuizi vya kupeleka vifaa vya kibinadamu kupitia njia pekee ya Semera-Abala-Mekelle kwenye mkoa wa Afar. Tangu tarehe 18 mwezi huu, msafara wa magari ya kusafirisha vifaa vya kibinadamu haukuingia mkoani Tigray. Kutokana na ukosefu wa mafuta, wenzi wengi wanaotoa misaada ya kibinadamu wamelazimika kupunguza au kusimamisha shughuli zao. Zaidi ya hayo, hali ya kibinadamu huko Afar na Amhara pia imekuwa mbaya zaidi kutokana na mapambano.