Kenya yahimiza jumuiya ya kimataifa iunge mkono matumizi ya programu za mabadiliko ya hali ya hewa ya Afrika
2021-10-27 09:14:01| cri

Kenya yahimiza jumuiya ya kimataifa iunge mkono matumizi ya programu za mabadiliko ya hali ya hewa ya Afrika_fororder_肯尼亚 气候变化

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya jana aliihimiza jumuiya ya kimataifa iunge mkono matumizi ya programu za mabadiliko ya hali ya hewa ya Afrika, hatua ambazo zitaisaidia Afrika kuimarisha uwezo wake wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Amesema ingawa kuna changamoto katika kutekeleza programu hizo, lakini matumizi yake yana maana sana. Pia ameonya kuwa bila ya matumizi ya programu hizo pato la taifa la Afrika litapungua kwa asilimia 30 hadi ifikapo mwaka 2050. Kenyatta amesema ingawa Kenya imeongeza utoaji wa fedha kwa ajili ya programu hizo katika miaka ya hivi karibuni, lakini bado inahitaji uungaji mkono zaidi kutoka jumuiya ya kimataifa.