Kiwango cha maambukizi ya malaria nchini Kenya chapungua kutokana na hatua imara za kuzuia
2021-10-28 09:39:49| cri

Kenya imesema kiwango cha maambukizi ya malaria ambacho kilikuwa kikubwa katika miaka ya nyuma sasa kimepungua kutokana na kuwekeza katika hatua imara za kuzuia.

Hayo yamesemwa na Katibu mkuu mtendaji wa Wizara ya Afya Mercy Mwangangi wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Utafiti wa Viashiria vya Malaria wa Kenya (KMIS) 2020 mjini Nairobi. Ameongeza kuwa mzigo wa malaria umepungua kutoka asilimia 8 ya mwaka 2015 hadi asilimia 6 ya mwaka 2020. Ametaja uungaji mkono endelevu na kampeni za kubadilisha tabia zinazolenga watu walio hatarini pia zimepelekea kuchukua hatua za kuzuia na kudhibiti katika ngazi ya jamii.

Mkuu wa Kitengo cha Taifa cha Mpango wa Malaria katika Wizara Afya, George Githuka amesema Kenya inajitahidi zaidi ili kuwa na angalau asilimia 80 ya wanawake wote wajawazito wanaoishi kwenye maeneo yenye magonjwa kupata angalau dozi tatu za dawa na kuendelea kufuata sera za ulinzi kwenye maeneo yasiyo na magonjwa.