Mjumbe wa China: Ushirikiano kati ya UM na AU ni muhimu zaidi kuliko hapo awali
2021-10-29 09:38:41| cri

Mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Zhang Jun amesema kuwa ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa (UM) na Umoja wa Afrika (AU) ni muhimu zaidi kuliko hapo awali kwenye mazingira ya mabadiliko makubwa katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na kijamii duniani na barani Afrika, pamoja na changamoto mpya.

Bw. Zhang ametoa wito wa ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na AU katika nyanja nne: kuisaidia Afrika kukabiliana na janga la COVID-19, kuisaidia Afrika kutatua matatizo makubwa ya amani na usalama, kuisaidia Afrika kushughulikia chanzo cha migogoro, na kuunga mkono nguvu za Afrika katika umoja.