AIIB yaidhinisha Nigeria kuwa mwanachama mpya
2021-10-29 09:39:03| cri

Benki ya Uwekezaji wa Miundombinu ya Asia (AIIB) imeidhinisha ombi la Nigeria la kujiunga na benki hiyo na kufanya idadi ya jumla ya wanachama wake kufikia 104, miongoni mwao nchi 11 ni kutoka Afrika.

Wanachama wa AIIB wa Afrika wanawajibika na asilimia zaidi ya 60 ya pato la taifa la bara hilo. Wanawakilisha asilimia zaidi ya 46 ya idadi ya watu wa Afrika.

Makamu rais wa AIIB ambaye pia ni katibu mkuu wa benki hiyo Bw. Ludger Schuknecht amesema kuwa kama benki ya maendeleo ya pande nyingi yenye azma ya kutoa mikopo endelevu ya fedha, AIIB inawapa wanachama wa Afrika fursa ya kupata mtaji wa bei nafuu na utaalamu wa miundombinu ili kusaidia kukabiliana na pengo hili.

Ameongeza kuwa wanatarajia kuunda uhusiano wenye nguvu zaidi na wanachama wapya barani Afrika na kushirikiana pamoja ili kufikia maendeleo endelevu ya muda mrefu.

Aidha AIIB ina wanachama wengine tisa kutoka Afrika wanaotarajiwa kujiunga na benki hiyo.