AfDB: Uchumi wa Afrika Mashariki watarajiwa kukua kwa asilimia 4.1 mwaka huu
2021-10-29 09:43:15| cri

AfDB: Uchumi wa Afrika Mashariki watarajiwa kukua kwa asilimia 4.1 mwaka huu_fororder_东非经济

Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB imesema uchumi wa Afrika Mashariki unatarajiwa kukua kwa asilimia 4.1 mwaka huu, likiwa ni ongezeko kutoka asilimia 0.4 ya mwaka jana.

Kwa mujibu wa Makadirio ya Uchumi wa Kanda ya Afrika Mashariki kwa mwaka 2021, hali ya uchumi wa kanda hiyo itakwenda sambamba na ufufukaji unaoendelea wa uchumi wa dunia. Hata hivyo Benki hiyo imesema kucheleweshwa kwa usambazaji wa chanjo dhidi ya COVID-19 na hatari za kuibuka kwa maambukizi kunaweza kupelekea ukuaji halisi wa uchumi kuwa chini kuliko ilivyokadiriwa.

Ripoti hiyo imepitia hali ya uchumi wa nchi zikiwemo Burundi, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Sudan, Tanzania na Uganda.