Afisa wa Sudan abainisha mipango na upatanishi ili kurejesha maelewano kati ya washirika
2021-10-29 09:41:05| cri

Afisa anayeshughulikia masuala ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan Ali Al-Sadiq amebainisha mipango na upatanishi ili kurejesha maelewano kati ya washirika wa kipindi cha mpito.

Ali Al-Sadiq amesema anakaribisha mpango wowote unaolenga kuondoa tofauti kati ya wapinzani. Pia amesisitiza kwamba vikosi vya ulinzi havina nia ya kuchukua madaraka, ambapo madaraka yatakabidhiwa kwa serikali itakayochaguliwa mwishoni mwa kipindi cha mpito. Oktoba 25 jeshi la Sudan lilipitisha hatua za kumaliza ushirikiano kati ya jeshi na muungano wa raia ambao ulikuwa ukitumikia utawala wa kipindi cha mpito.