Rais wa China atoa wito wa kutekeleza kikamilifu Mkataba wa UM wa Mabadiliko ya Tabianchi
2021-10-31 21:51:56| Cri

Rais Xi Jinping wa China ametoa wito wa kutekeleza kikamilifu na kwa ufanisi Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi na Mkubaliano ya Paris chini yake, na kusema ni lazima kuzingatia hadhi ya Umoja wa Mataifa kama njia kuu, kufuata msingi wa kubeba wajibu wa pamoja lakini pia ulio tofauti, na sheria za kimataifa, kuchukua hatua zenye ufanisi ili kuinua kiwango cha ushirikiano.

Xi alisema hayo alipoendelea kushiriki kwa njia ya video Mkutano wa 16 wa viongozi wa nchi za Kundi 20.

Wakati wa mkutano huo, Xi pia ameeleza kuwa katika miaka ya hivi karibuni, maafa makubwa yanatokea mara kwa mara, hali ambayo inaharakisha mchakato wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. Ni lazima kuratibu hatua za ulinzi wa mazingira na maendeleo ya uchumi, ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi huku maisha ya watu yakihakikishwa.

Xi amesema, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kutimiza mageuzi ya matumizi ya nishati kunategemea maendeleo ya tekonojia. Nchi za G20 zinapaswa kuongoza kuhimiza matumizi ya teknolojia ya kisasa. Nchi zilizoendelea pia zinatakiwa kutekeleza ahadi zao, na kuzitolea nchi zinazoendelea msaada wa kifedha.

Pia amesisitiza kuwa, mabadiliko ya tabianchi na suala la nishati ni changamoto kubwa zinazoikabili dunia, na yanahusiana na maslahi ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa na mustakabali wa dunia. Jumuiya ya kimataifa inapaswa kuchukua hatua halisi katika kukabiliana na changamoto hizo.