Mji wa Cape Town wamtunuku cheti cha heshima mkazi wake mchina
2021-11-01 09:16:38| CRI

Meya wa mji wa Cape Town Bw. Alderman Dan Plato jana alimtunuku cheti cha heshima Bw. Hu Jianhua ambaye amekuwa akiishi mjini Cape Town kwa karibu miaka 30, kutokana na mchango wake kwenye mambo ya kibinadamu na uchumi kwa mji huo.

Akiongea baada ya kumtunuku cheti hicho, Meya Dan Plato amesema Bw. Hu amekuwa mtu muhimu kwenye kujenga uhusiano kati ya China na mji wa Cape Town, na kupongeza mchango wake. Meya huyo pia amesema cheti hicho pia ni kwa ajili ya jumuiya yote ya wachina, ambayo imetoa mchango ikiwa ni pamoja na pesa na vifaa, ili kuusaidia mji wa Cape Town na miji mingine kwenye jimbo la Western Cape, kupambana na COVID-19.

Meya Dan Plato pia ameishukuru konseli kuu ya China mjini Cape Town kwa mchango wake wakati wa janga la hilo.