Chama tawala cha Zimbabwe champitisha Bw. Mnangagwa kuwa mgombea urais wa chama hicho
2021-11-01 09:29:58| CRI

Chama tawala cha Zimbabwe ZANU-PF kimemwidhinisha rais wa sasa wa nchi hiyo Bw. Emmerson Mnangagwa kuwa mgombea urais wa chama hicho kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2023.

Uamuzi huo uliotolewa Jumamosi wiki iliyopita katika mkutano wa mwaka wa chama hicho huko mji wa Bindura, umeungwa mkono kwa kauli moja baada ya kuzingatia kazi zilizofanywa na Bw. Mnangagwa kuendeleza nchi tangu awe rais wa Zimbabwe mwaka 2018.

Kaimu msemaji wa chama hicho Mike Bimha amesema mkutano huo umeazimia kuongeza nguvu kwa chama hicho, ili kujiandaa kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2023.