Ethiopia yawaua washukiwa 170 wa kundi la waasi
2021-11-01 12:04:58| CRI

Shirika la habari la serikali ya Ethiopia (ENA) limesema kikosi cha usalama cha jimbo la Oromia nchini Ethiopia kimewaua watuhumiwa 170 wenye uhusiano na kundi la waasi la Oromo Liberation Army (OLA).

Habari zinasema watuhumiwa 12 wa kundi hilo na wengine 51 wanaoshukiwa kuwa washirika wao pia walikamatwa katika operesheni.

Kundi la OLA ni kundi la tawi la waasi la zamani la Oromo Liberation Front (OLF) ambalo ni chama cha upinzani kinachodai kupigania haki za kabila la Oromo ambao ni asilimia 35 ya watu wa Ethiopia.