Kenya yaahidi kubeba jukumu katika kukuza amani, usalama barani Afrika
2021-11-02 09:07:38| CRI

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema nchi yake itatumia nafasi yake kama mwanachama asiye wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kukuza amani, utulivu na ukuaji jumuishi katika Afrika.

Kwenye hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na waziri wa Ulinzi Eugene Wamalwa katika mkutano wa kikanda ulioandaliwa na Umoja wa Afrika, rais Kenyatta amesema Kenya imejihusisha zaidi katika diplomasia ya kukuza amani, kulinda usalama, kutatua migogoro na kuhimiza ujenzi baada ya migogoro katika Afrika.

Mkutano huo wa 12 ambao ni wa ngazi ya juu na kujikita kwenye kukuza amani, usalama na utulivu, unahudhuriwa na maafisa waandamizi wa serikali wakiwemo mabalozi na viongozi wa zamani wa Afrika.