Somalia yaanza kufanya uchaguzi wa baraza la chini la bunge
2021-11-02 09:47:21| CRI

Somalia imeanza uchaguzi wa baraza la chini la bunge Jumatatu wiki hii ambapo wagombea wawili kutoka Somaliland kati ya wanne wameshinda viti kwenye uchaguzi huo.

Waziri mkuu wa nchi hiyo Mohamed Hussein Roble amepongeza wabunge hao wawili kushiriki kwenye bunge na kuhimiza majimbo mengine nchini humo kuharakisha mchakato wa uchaguzi husika.

Wabunge hao watachaguliwa kwa pamoja na asasi za kiraia, wazee wa kimila na serikali za majimbo ambapo uchaguzi huo utafanyika katika sehemu mbili tu katika kila jimbo, zikipungua kutoka nne kulingana na zamani.

Wajumbe 54 wa Seneti na wabunge 275 wa baraza la chini la bunge wanatarajiwa kuchagua rais mpya kwa pamoja baadaye mwaka huu au mapema mwaka kesho.