Majangili zaidi ya 200 wakamatwa katika hifadhi ya taifa ya Ruaha nchini Tanzania mwaka 2020/21
2021-11-02 09:49:05| cri

Majangili na wavuvi haramu wasiopungua 230 wamekamatwa katika kipindi cha mwaka 2020/21 kwenye hifadhi ya taifa ya Ruaha nchini Tanzania, ambayo ni hifadhi kubwa zaidi nchini humo yenye eneo la kilomita za miraba 20,226.

Afisa uhifadhi wa kitengo cha utalii na usalama katika Hifadhi ya Ruaha Jackson Laizer alisema kuwa wahalifu hao walikamatwa chini ya operesheni iliyoungwa mkono na serikali ya kupambana na ujangili. Amebainisha kuwa ingawa sasa ujangili wa tembo umedhibitiwa, lakini changamoto za uwindaji kwa ajili ya kupata nyama na uvamizi wa wafugaji wanaotafuta malisho ya mifugo yao bado zipo.