CMG yatoa pendekezo la kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
2021-11-03 15:21:47| CRI

CMG yatoa pendekezo la kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi_fororder_微信图片_20211103152119

Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi unafanyika mjini Glasgow, Uingereza. Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) limetoa Pendekezo la Mwaka 2021 la Dunia Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi.

Vipindi maalum vya televisheni vya CMG kuhusu pendekezo hilo vimezinduliwa jana, na vitaendelea kwa siku tano, ambapo viongozi wa nchi na mashirika mbalimbali ya kimataifa wamehudhuria majadiliano kwenye vipindi hivyo.

Mkuu wa CMG Shen Haixiong alipohutubia uzinduzi wa vipindi hivyo amevihimiza vyombo vya habari duniani vibebe majukumu, na kuhimiza hatua halisi kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi duniani.

Kwenye hotuba yake rais Julius Maada Bio wa Sierra Leone amesema mabadiliko ya tabianchi ni changamoto ya pamoja ya binadamu wote, dunia inapaswa kushikamana ili kukabiliana na changamoto hiyo.