Tembo waharibu ekari 250 za mashamba ya mazao kaskazini mwa Tanzania
2021-11-03 09:21:37| CRI

Kundi la tembo 70 limevamia vijiji vya wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, Tanzania na kuharibu jumla ya ekari 250 za mashamba ya mazao ya wanakijiji.

Akiongea kwenye mkutano wa madiwani wa mkoa wa Manyara, diwani wa Ngorika Albert Msole amesema, tembo hao wavamizi wamekuwa wakifanya uharibifu kwenye vijiji kadhaa vya wilaya kwa muda, na wanavijiji wamepoteza kiasi cha ekari 250 za mazao yao shambani. Amezitaka mamlaka za wanayamapori kuwafukuza wanyama hao ambao wanaripotiwa kutoroka kwenye Mbuga ya Taifa ya Ziwa Manyara, kabla ya kusababisha uhabirifu mkubwa zaidi kwenye vijiji hivyo.

Mwanakijiji mmoja aitwaye Athuman Iddi amesema tembo wameharibu ekari tano za shamba lake la mahindi, na kutishia usalama wa chakula nyumbani kwake.