Chama cha wafanyabiashara Kenya chazindua huduma ya eskro ili kupambana na utapeli wa kuvuka mpaka wa mtandaoni
2021-11-03 09:30:21| CRI

Chama cha Kitaifa cha Biashara na Viwanda cha Kenya (KNCCI), ambayo ni taasisi mwavuli kwa wajasiriamali wa nchi hiyo, jana Jumanne kilizindua huduma ya eskro (escrow service) ili kuwalinda wafanya biashara ya mtandaoni ya ndani na ya kuvuka mpaka dhidi ya utapeli.

Mwenyekiti wa chama hicho Richard Ingatia amesema huduma hiyo inahusisha akaunti ya eskro ambayo itahifadhi pesa za malipo za wanunuzi hadi miamala itakapomalizika kwa mafanikio.

Ngatia amesema huduma hiyo imetolewa wakati mzuri ambapo miamala mingi ya biashara imekuwa inafanyika kupitia mtandao kutokana na janga la Corona.