Kampuni ya China yachangia kompyuta katika Chuo Kikuu cha Zambia
2021-11-03 10:01:00| cri

Kampuni ya Taiji ya China inayoshughulikia teknolojia ya elektroniki (CETC) Jumanne wiki hii ilichangia kompyuta 10 katika Chuo Kikuu cha Zambia (UNZA) ambacho ni chuo kikubwa zaidi cha serikali nchini humo. Kompyuta hizo zimepatiwa idara ya sayansi ya kompyuta kwa ajili ya kusaidia kuhimiza kutoa maarifa juu ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA).

Makamu Chansela wa chuo hicho Bw. Luke Mumba aliishukuru kampuni hiyo kwa mchango wake ambao utainua kiwango chake cha elimu ya teknolojia haswa katika kipindi ambacho serikali ya Zambia imepanga kuhimiza mageuzi ya kidigitali na kuendeleza uchumi katika sekta husika huku wahitimu wa fani hiyo wakihitajika.

Pia Bw. Mumba aliongeza kuwa makubaliano ya maelewano yaliyosainiwa mwaka 2019 kati ya chuo hicho na kampuni hiyo juu ya kufadhili ujenzi wa kituo cha Tehama, imethibitisha tena utekelezaji wa ushirikiano kati ya China na Zambia katika kuhimiza mpango wa Zambia wa kuboresha mageuzi ya kidigitali.