UM walaani shambulizi lililowajeruhi walinda amani 10 nchini CAR
2021-11-03 15:19:23| CRI

Naibu msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Farhan Haq jana alisema kuwa Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (MINUSCA) imelaani vikali shambulio lililofanywa na askari wa kikosi cha ulinzi wa rais na kuwajeruhi askari 10 wa kulinda amani.

Msemaji huyo alisema shambulio hilo dhidi ya askari wa kulinda amani wa Misri ambalo limesababisha kifo cha raia mmoja, linaonekana kufanywa kwa makusudi na haliwezi kusamehewa.

Uongozi wa MINUSCA na serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati walifanya mazungumzo mara moja ili kuanza uchunguzi wa tukio hilo na kuhakikisha wahusika wanawajibishwa kwa mujibu wa makubaliano kati ya Umoja wa Mataifa na serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.