China na Zambia zaahidi kuhimiza ushirikiano katika sekta ya elimu
2021-11-04 09:58:43| cri

China na Zambia zimeahidi kuhimiza ushirikiano kati yao katika sekta ya elimu. Ahadi hiyo imetolewa wakati Balozi wa China nchini Zambia Li Jie alipokutana na Waziri wa Elimu wa Zambia Douglas Syakalima wiki hii.

Balozi Li alieleza kuwa China imetekeleza miradi mbalimbali ya elimu nchini Zambia ili kusaidia vijana kupata elimu na ufundi unaohitajika kwa ajira ya kazi zao. Ubalozi wa China unaendelea kufadhili wanafunzi hodari wa vyuo waliosomea kwenye mazingira magumu, kupitia Udhamini wa Masomo wa Balozi. Na China imekuwa nchi maarufu wanayokwenda kusoma wanafunzi wa Zambia.

Kwa upande wake Waziri Syakalima alishukuru uungaji mkono wa muda mrefu wa China katika sekta husika haswa katika mafunzo ya wanafunzi wenye vipaji, ufundi na kubadilishana kati ya wasomi. Aliongeza kuwa Zambia inapenda kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kielimu na China.