Serikali ya Senegal yatoa nishani kwa wahudumu wote wa timu ya matibabu ya China
2021-11-04 09:53:44| CRI

Serikali ya Senegal jana ilitoa nishani na vyeti vya heshima kwa wahudumu wote wa timu ya 18 ya misaada ya matibabu ya China ili kusifu mchango wao mkubwa kwa sekta ya matibabu na afya ya Senegal.

Siku hiyo mwakilishi wa wizara ya afya na huduma za kijamii ya Senegal, Bw. Mamadou Ramin Baki aliipongeza timu hiyo na kuwashukuru madaktari kwa kutoa matibabu kwa watu wa Senegal, akisifu ustadi bora na maadili mema ya timu hiyo.

Mjumbe wa ubalozi wa China nchini Senegal Bw. Zhao Yunchun alisema kuwa, timu hiyo ilifanya juhudi kukabiliana na janga la COVID-19 na kutoa uzoefu mzuri wa China wa kupambana na janga hilo, ikishirikiana na watumishi wa afya wenyeji kutoa huduma za afya kwa wagonjwa.