Tanzania yasajili miradi ya uwekezaji yenye thamani ya dola bilioni 3.5 za kimarekani ndani ya miezi saba
2021-11-04 10:32:06| CRI

Serikali ya Tanzania imesema, kuanzia Aprili hadi Oktoba mwaka huu, imesajili miradi 182 yenye thamani ya dola bilioni 3.5 za kimarekani.

Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia uwekezaji Bw. Geoffrey Mwambe amesema, miradi 164 kati ya 182 ya uwekezaji ilisajiliwa na Kituo cha Uwekezaji cha Tanzania (TIC) na miradi mingine 18 ilisajiliwa na Mamlaka ya Eneo la Kushughulikia Mauzo nje (EPZA).

Bw. Mwambe amesema, miradi 182 ya uwekezaji iliyosajiliwa katika miezi saba iliyopita inatarajiwa kutoa nafasi 48,000 za ajira kwa watanzania.

Amesema, miradi mingi ya uwekezaji iliyosajiliwa inahusisha sekta za kilimo, ujenzi, utengenezaji na viwanda na uchimbaji wa madini.