Makampuni ya Biashara ya China yachangia chakula kwa viongozi wa kata nchini Rwanda
2021-11-04 09:39:11| CRI

Wafanyakazi wa Shirikisho la Makampuni ya Biashara na Shirikisho la Wachina nchini Rwanda jana Jumatano walichangia vyakula vya aina mbalimbali kwenye kata ya Kimiroko, moja ya kata zinazounda wilaya ya Gasabo ya mjini Kigali, ili kusaidia familia zilizoathirika na janga la COVID-19.

Mchango huo wa chakula ambao unajumuisha vipolo vya mchele na unga wa mahindi, pamoja na mafuta ya kupikia ulikabidhiwa kwa mamlaka za kata ya Kimironko mjini Kigali. Akishukuru kutolewa kwa msaada huo, naibu mkuu wa wilaya ya Gasabo, Regis Mudaheranwa amesema wanatarajia kuanzisha uhusiano na ushirikiano wa kikazi na Shirikisho la Wachina, ambapo wilaya yake ipo tayari na imedhamiria kuyasaidia makampuni ya biashara ya China nchini Rwanda wakati wowote yanapohitaji huduma inayohusiana na biashara yao.

Amesema misaada hiyo itatolewa kwa familia zenye mazingira magumu za kata ya Kimironko ambazo zimeathiriwa na janga la COVID-19, hasa zenye wagonjwa wa COVID-19 ambao wako nyumbani.