China yaendelea kuwa nchi kubwa ya kwanza kwa uuzaji nje wa Namibia mwezi Septemba
2021-11-04 09:59:15| cri

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Shirika la Takwimu la Namibia (NSA), China imeendelea kuwa nchi kubwa ya kwanza kwa Namibia kuuza bidhaa zake nje katika mwezi Septemba mwaka huu, ambapo imesafirisha asilimia 34.6 ya bidhaa zake nchini China. Nchi nyingine nne zikiwemo Afrika Kusini, Bostwana, Hispania na Zambia pia zimeorodheshwa kwenye nchi tano kubwa zaidi kwa uuzaji nje wa Namibia.