Watafiti wa Afrika Kusini wagundua fuvu la mtoto lenye miaka zaidi ya 250,000 iliyopita
2021-11-05 09:39:05| CRI

Timu ya watafiti kutoka chuo kikuu cha Witwatersrand na vingine 13 vya Afrika Kusini jana Alhamis vilitangaza kugundua sehemu za fuvu na meno ya mtoto aliyefariki miaka 250,000 iliyopita ambapo amekadiriwa kuwa na miaka 5 au 6.

Kiongozi wa timu ya utafiti Lee Rogers, ambaye ni mkurugenzi wa Kituo cha Uchunguzi wa Safari ya Kina ya Binadamu (Centre for Exploration of the Deep Human Journey) cha chuo kikuu cha Witwatersrand amesema sehemu za fuvu la Homo naledi zilipatikana kwenye eneo la urithi wa dunia la Cradle Humankind karibu na Johannesburg. Homo neledi ni spishi ya binadamu wa kale iliyogunduliwa kwenye pango la Rising Star katika miaka 335,000 hadi 236,000 iliyopita.

Kwa mujibu wa Berger, vipande 2,000 vya watu zaidi ya dazeni mbili katika hatua zote za maisha za Homo naledi vimegunduliwa tangu ugunduzi wa kwanza uliofanyika mwaka 2013.