Kenya yaunda tume ya kuboresha usalama wa mtandaoni
2021-11-05 09:39:37| CRI

Kenya jana Alhamis ilizindua tume ya kusaidia kuboresha usalama mtandaoni wa kuvuka mpaka.

Waziri wa Mambo ya Ndani Fred Matiang’i amesema Tume ya Kompyuta ya Taifa na Uratibu wa Uhalifu wa Mtandaoni (NCCCC) itaweka kipaumbele kwenye matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii ambayo ameelezea kama tishio kubwa la usalama wa taifa na mafungamano, na kuapa kwamba kutakuwa na msako mkali na endelevu dhidi ya wahalifu hasa katika kipindi cha uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti mwakani.

Amesema uwekezaji kwenye sekta ya usalama wa mtandaoni ambao thamani yake ni shilingi bilioni 13 za Kenya utasaidia kuiweka Kenya sawa na nchi nyingine duniani kwenye masuala ya usalama wa mtandaoni.