Tume ya UM nchini DRC yachukua tahadhari baada ya waasi kuvamia mji wa mashariki
2021-11-05 09:35:31| CRI

Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUSCO) inachukua tahadhari kufuatia kundi la waasi kuvamia mji wa mashariki wa Bukavu mapema Jumatano.

Maofisa wa huko wamesema, kundi la waasi walishambulia baadhi ya maeneo ya mji wa Bukavu mkoani Kivu Kusini, vikiwemo vituo vya kijeshi, ambapo washambuliaji sita, askari wawili na polisi mmoja waliuawa kwenye tukio hilo.

Msemaji wa MONUSCO Mathias Gillman amesema tume hiyo inafuatilia kwa karibu hali ya sasa, na polisi na vikosi vya Umoja wa Mataifa wako kwenye tahadhari ya juu wakidumisha mawasiliano ya karibu na serikali ya mkoa huo.

Kwa mujibu wa msemaji huyo, washambuliaji 36 wamekamatwa, na uchunguzi bado unaendelea ili kuwatambua.