Somalia yamwamuru mwanadiplomasia wa AU kuondoka Mogadishu
2021-11-05 09:48:43| CRI

Serikali ya Somalia jana ilimwamuru mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa tume ya kulinda amani ya Umoja ya Afrika nchini Somalia (AMISOM) kuondoka nchini humo ndani ya siku saba.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ilimtangaza naibu mwakilishi maalum wa tume hiyo Bw. Simon Mulongo kuwa mtu asiyekaribishwa, ikisema mwanadiplomasia huyo alikuwa akishughulikia mamlaka asiyokabidhiwa na tume hiyo. Wizara hiyo ilisema kuwa imemuamuru Bw. Mulongo kuondoka nchini Somalia ndani ya siku saba kutokana na kujihusisha na mambo yasiyoendana na mamlaka ya AMISOM na mkakati wa usalama wa Somalia.