Wapiganaji 12 wa kundi la al-Shabab wakamatwa kusini mwa Somalia
2021-11-08 11:58:45| CRI

Vikosi vya usalama vya Somalia Jumapili vimewakamata wapiganaji 12 wa Kundi la al-Shabab katika mji mkuu wa Jimbo la Kusini Magharibi, Baidoa nchini humo.

Kamanda wa Shirika la Ujasusi na Usalama la jimbo hilo Mohamud Mohamed Hassan amesema, katika operesheni hiyo, vikosi hivyo vilifanikiwa kuharibu mtandao wa kigaidi, na kuongeza kuwa, wapiganaji hao walijaribu kuleta hofu na vitisho mjini Baidoa kabla ya kukamatwa.

Operesheni hiyo imefanyika kabla ya uchaguzi wa wabunge katika Jimbo la Kusini Magharibi.