Waethiopia waandamana kupinga uingiliaji wa kigeni
2021-11-08 08:58:06| cri

Maelfu ya Waethiopia wamekusanyika katika Uwanja wa Meskel katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, wakipinga uingiliaji wa kigeni na shinikizo katika masuala ya ndani ya nchi hiyo.

Akizungumza na umati huo, Meya wa jiji la Addis Ababa, Adanech Abiebi amesisitiza kuwa, sio shinikizo la pande zote la kigeni wala shambulizi la waasi litakalowazuia Waethiopia kutimiza matarajio ya maendeleo ya nchi hiyo.

Amesema lengo lililofichika la uingiliaji wa kigeni na shinikizo la pande zote kwa Ethiopia ni kulifanya taifa hilo kutii matakwa ya nchi za kigeni, na kusisitiza kuwa, Waethiopia watakwepa uingiliaji wowote na shinikizo la kigeni na kusimama pamoja kwa umoja.

Maandamano hayo yamefanika siku chache baada ya Bunge la Ethiopia kuidhinisha amri ya kipindi cha hali ya hatari kitakachodumu kwa miezi sita kutokana na kuongezeka kwa mapigano katika sehemu ya kaskazini mwa nchi hiyo.