Rwanda yapokea shehena ya pili ya chanjo ya COVID-19 kutoka China
2021-11-08 08:58:45| cri

Rwanda imepokea shehena ya pili ya chanjo ya virusi vya Corona iliyotolewa na serikali ya China.

Mkuu wa Idara ya Kudhibiti na Kukinga Magonjwa iliyo chini ya Kituo cha Madawa Cha Rwanda Albert Tuyishime amesema, msaada huo ni alama ya uratibu na uungaji mkono wa serikali ya China katika mapambano dhidi ya janga hilo. Amesema Rwanda inaichukulia China kama kiongozi katika kuchochea upatikanaji wa usawa wa chanjo ya virusi vya Corona, na kuzitaka nchi nyingine kubwa kuunga mkono ili nchi nyingi ziweze kupata chanjo.

Naye Mshauri wa uchumi na biashara katika Ubalozi wa China nchini Rwanda, Wang Jiaxin amesema, China inafurahi kuchangia utoaji wa chanjo nchini Rwanda, na msaada huo unaonyesha mshikamano na urafiki kati ya nchi hizo mbili.