Mkuu wa jeshi la Sudan aahidi kujitolea kutimiza mpito wa kidemokrasia
2021-11-08 08:56:40| cri

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Sudan Jenerali Abdel Fattah Al-Burhan jana amerejea tena ahadi yake ya kutimiza mpito wa kidemokrasia nchini humo.

Al-Burhan amesema hayo jana alipopokea ujumbe wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu ulioongozwa na naibu katibu mkuu wa Jumuiya hiyo, Hossam Zaki. Amesema, jeshi la nchi hiyo limejitolea kusimamia mpito wa kidemokrasia hadi serikali mpya itakayochaguliwa na watu kuingia madarakani.

Kwa upande wake, Bw. Zaki amesema Jumuiya hiyo inapenda kusaidia kuhimiza pande za Sudan kufanya mazungumzo, ambayo ni muhimu katika kufikia suluhisho litakaloridhisha pande zote.