Mtaalamu wa Kenya asema China yachochea uhai katika mageuzi ya kijani ya Afrika
2021-11-09 08:57:23| cri

Mtaalamu wa Kenya asema China yachochea uhai katika mageuzi ya kijani ya Afrika_fororder_iJfvAF2-_400x400

Mtaalamu wa masuala ya uhusiano wa kimataifa kutoka nchini Kenya, Adhere Cavince amesema, China, ikiwa mwenzi mkubwa na chanzo muhimu cha uwekezaji wa moja kwa moja barani Afrika, imeweka uhai katika mchakato wa bara hilo kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Amesema mchakato wa kupunguza utoaji wa hewa chafu barani Afrika umeongezeka kwa kasi kutokana na fedha, ufundi na uhamishaji wa teknolojia kutoka China.

Adhere amesema China imekuwa mstari wa mbele katika mabadiliko ya kupunguza utoaji wa hewa chafu na njia za maendeleo endelevu barani Afrika, ambako mabadiliko ya tabianchi yameleta athari kubwa katika maisha na mifumo muhimu ya ikolojia.

Amesema mkutano ujao wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) utakaofanyika mjini Dakar, Senegal, utatoa jukwaa la kutafuta njia za uvumbuzi zitakazosaidia mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.