Jeshi la DRC ladai waasi wa kundi la M23 wanashambulia vituo vya jeshi
2021-11-09 08:55:56| cri

Jeshi la ulinzi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) limelituhumu kundi la M23 kwa kufanya mashambulizi katika eneo la mpaka wa kaskazini mashariki mwa nchi hiyo na Uganda, ambako vurugu zimeongezeka mwaka huu kutokana na uwepo wa makundi mengi yenye silaha.

Katika taarifa yake, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi hilo Celestin Mbala Munsense amesema, waasi hao wameshambulia vituo vya jeshi vilivyoko Chanzu na Runyonyi na maeneo mengine katika mkoa wa Kivu Kaskazini kwa lengo la kuvuruga usalama na utulivu.

Hata hivyo, kiongozi wa kundi la M23 Betrand Bisimwa amekana kuwa wafuasi wake wamefanya mashambulizi katika mkoa huo.