AU yataka majadiliano ya maana na kweli yafanyike kutafuta suluhisho la kudumu nchini Ethiopia
2021-11-10 08:31:30| CRI

AU yataka majadiliano ya maana na kweli yafanyike kutafuta suluhisho la kudumu nchini Ethiopia_fororder_Flag_of_the_African_Union.svg

Umoja wa Afrika (AU) umezitaka pande zinazohusika katika mapigano nchini Ethiopia kufanya majadiliano ya maana ili kupata suluhisho la kudumu la mgogoro unaoendelea nchini humo.

Taarifa hiyo imetolewa na Baraza la Amani na Usalama la Umoja huo jana jumanne kufuatia mkutano wa Baraza hilo uliofanyika jumatatu kujadili hali ya sasa ya nchini Ethiopia.

Huku likisisitiza umuhimu wa majadiliano ya kina, jumuishi, na ya kitaifa ili kudumisha amani, utulivu, demokrasia, utawala bora na maridhiano nchini Ethiopia, Baraza hilo limeeleza kuunga mkono kithabiti juhudi za Mwakilishi wa Ngazi ya Juu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika, Olusegun Obasanjo katika kusimamisha vurugu na kutafuta suluhisho la Amani la mgogoro huo, na kukaribisha juhudi za kikanda na kimataifa katika kutimiza lengo hilo.

Baraza hilo pia limesisitiza kuwa, kuongezeka kwa mapigano kuna athari kubwa kwa Amani, usalama na utulivu wa Ethiopia na kanda hiyo, pia kuna athari kubwa kwa hali ya kibinadamu na kisiasa.