Afrika na China zapaswa kufanya juhudi kwa pamoja kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja kati ya China na Afrika
2021-11-10 09:54:02| cri

Waziri wa Mambo ya Nje wa Senegal Bw. Essata Tale Sall amesema, nchi za Afrika na China zinapaswa kulinda na kuimarisha Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), na kujitahidi kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja kati ya China na Afrika katika zama mpya.

Habari zinasema, mkutano wa 8 wa Mawaziri wa FOCAC utafanyika kuanzia tarehe 29 hadi 30 mwezi huu huko Dakar, Senegal.

Bibi Essata amesema, anatumai mkutano huo utajadili kwa kina suala la kuhimiza ufufukaji wa uchumi, afya, ujenzi wa miundombinu na kadhalika, kuimarisha ushirikiano kati ya Afrika na China katika miaka mitatu ijayo.