Watu 11 wauawa katika shambulizi dhidi ya msikiti mmoja kaskazini magharibi mwa Nigeria
2021-11-11 08:22:43| cri

Watu 11 wauawa katika shambulizi dhidi ya msikiti mmoja kaskazini magharibi mwa Nigeria_fororder_webwxgetmsgimg (2)

Polisi nchini Nigeria wamethibitisha kwamba, watu 11 wameuawa na wengine wanane kujeruhiwa baada ya watu wasiojulikana waliokuwa na silaha kushambulia msikiti mmoja kwenye jimbo la Katsina, kaskazini magharibi mwa Nigeria.

Msemaji wa Polisi wa jimbo hilo, Bw. Gambo Issa amesema, watu kadhaa waliokuwa na silaha walivamia msikiti katika mji wa Bachari jioni ya tarehe 9 na kuwashambulia kwa risasi watu waliokuwa katika ibada. Polisi wameanza kuchunguza shambulizi hilo na kuwasaka wapiganaji hao.