Wataalamu wa EAC kutambua fursa za uwekezaji katika uzalishaji wa viua vijasumu (antibiotics)
2021-11-11 08:24:07| CRI

Wataalamu kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wameanza mkutano wa siku mbili mjini Arusha, Tanzania, unaolenga kutambua vivutio vya uwekezaki katika uzalishaji wa viua vijasumu (antibiotics) katika kanda hiyo.

Mkurugenzi wa sekta ya Uzalishaji katika Jumuiya hiyo, Jean Baptiste Havugimana amesema katika mkutano huo kuwa, sekta ya madawa ni moja ya maeneo ya vipaumbele katika sera ya viwanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Ameongeza kuwa, kanda hiyo ina nia ya kuendeleza sekta ya madawa kama sehemu ya ajenda ya maingiliano ya kijamii na kisiasa.