Madereva 72 wanaofanya kazi katika Shirika la WFP wawekwa kizuizini na serikali ya Ethiopia
2021-11-11 11:51:40| Cri

Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa huko Semela, Afar, kaskazini mwa Ethiopia, madereva 72 wenyeji wanaofanya kazi katika Shirika la Mpango wa Chakula Duniani waliwekwa kizuizini na serikali ya Ethiopia, na watu 6 waliachiliwa baadaye. Msemaji huyo wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa anawasiliana na serikali ya Ethiopia ili kujua sababu za kuzuiliwa kwao na anaiomba serikali ya eneo hilo kuhakikisha usalama wa wafungwa na kulinda haki zao za kisheria na haki za binadamu. Wafanyakazi husika wa serikali ya Ethiopia wamesema kuwa madereva hawa waliozuiliwa wanaweza kuwa na uhusiano na Kundi la Ukombozi wa Watu wa Tigray."

Tangu Ethiopia ilipoingia katika hali ya hatari mnamo tarehe 2 mwezi Novemba, kulingana na mswada uliotangazwa na nchi hiyo, watu wanaoshukiwa wanaweza kukamatwa bila ya hati ya kukamatwa.