Afrika yarekodi ukuaji mkubwa katika usafirishaji wa mizigo mwezi Septemba
2021-11-12 10:27:06| Cri

Afrika imeshuhudia ukuaji mkubwa katika kiwango cha usafirishaji wa mizigo duniani mwezi Septemba ikilinganishwa na kanda nyingine zote duniani, wakati ambapo mashirika ya ndege yanaendelea kufufuka kutokana na athari za COVID-19.

Takwimu zilizotolewa na Shirikisho la Usafiri wa Ndege Duniani (IATA) zinaonesha kuwa Afrika imerekodi asilimia 34.6 ya ukuaji katika kipindi cha mapitio na kufanya ukuaji kuendelea kwa miezi tisa mfululizo. Kwa mujibu wa IATA, kiwango hicho kiko juu kwa asilimia 20 kabla ya janga mwaka 2019, lakini kimekuwa kizuri zaidi katika miezi sita iliyopita.