Kikao cha ECA kuhusu uongozi chahimiza uchumi tofauti kwa eneo la katikati ya Afrika
2021-11-12 09:21:20| CRI

Nchi za kanda ya katikati ya Afrika zimepata maendeleo katika nia yao ya kutambua vyanzo tofauti vya ukuaji wa uchumi na kuboresha mazingira ya biashara, lakini zinapaswa kuongeza juhudi zaidi ili kuhimili athari kutokana na kutegemea zaidi nguvu za nje wakati wa mlipuko wa janga la virusi vya Corona.

Hayo yamesemwa na Ofisa Msimamizi wa Ofisi ya Kamati ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa (ECA) Kanda ya Afrika ya Kati, Jean Luc Mastaki, baada ya Kamati hiyo kutangaza mkutano wa 37 wa Kamati ya Maingiliano ya Kiserikali ya Maofisa Waandamizi na Wataalamu (ICE) wa Afrika ya Kati, uliopangwa kufanyika Brazzaville, Jamhuri ya Kongo, kuanzia Desemba 6 hadi 10 mwaka huu.

Amesema mkutano huo utajadili hali ya uongozi na mabadiliko katika kanda ya Afrika ya kati, kutambua mapungufu na kutoa mapendekezo kwa serikali na mashirika ya kikanda kuhusu hatua za kuongeza uelewa na vitendo halisi vya nadharia zinazoingiliana, ili kuongeza kasi ya uchumi anuai katika kanda hiyo.